Featured Kitaifa

CHATANDA AZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA,KATIMBA ATAJA NAMNA ITAKAVYOWAFIKIA WANAWAKE NA WATOTO

Written by mzalendoeditor
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizindua  kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu_DODOMA
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda ,amezindua kampeni ya msaada wa Kisheria inayoratibiwa na Kamati ya Haki na Sheria ya UWT yenye lengo la kuwasaidia wanawake na makundi maalum kupata haki ya msaada wa Kisheria nchini.
Bi.Chatanda akizungumza mara baada ya kuzindua kamati hiyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
Amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuunga mkono jitihada za awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid Chini ya Wizara ya Katiba na Sheria inayofanya vizuri kwa sasa.
“Kampeni hii ya utoaji wa msaada wa kisheria itakuwa inafanya kazi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yenye lengo la kutoa huduma za msaada wa kisheria  na kuhakikisha upatikanaji wa haki sawa kwa wote kwa kuzingatia zaidi wanawake ,wasichana,watu wanaoishi na ulemavu  na makundi mengine hatarishi,”amesema Bi.Chatanda
Amesema kuwa UWT pamoja na wadau wengine wanalenga kuhakikisha kwamba elimu ya kisheria  na msaada wa kisheria inafika kwa watu wote hasa wanawake  na makundi maalum.
“UWT inalenga kuchangia jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote kuhusiana na matatizo ya ardhi,matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake urithi,Ndoa,kesi za madai na jinai.”amesema
Aidha ametoa maagizo kwa makatibu wa mikoa na wilaya kama watendaji kutoa ushirikiano wa kutosha pindi zoezi hilo la utoaji msaada wa kisheria litakapoaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi  na kuhakikisha ripoti ya uendeshaji wa zoezi hilo.
Pia ametoa rai kwa wananchi hasa wanawake nchini kutumia fursa hiyo ya utoaji wa msaada wa kisheria ambayo imekwenda kuanza leo hapa Dodoma na baadae kwenye mikoa yote nchini kwa siku zijazo.ambapo kwenye viwanja vya Chinangali itakwenda kufanyika leo na kesho Septemba 8,2024.
kwa upande wake  Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Naibu Waziri TAMISEMI, Zainab Katimba amesema imeanzishwa kampeni ya msaada wa kisheria itakayoanza kwenye mikoa 10 na kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kwenye ofisi za UWT kutakuwa na watoa msaada kisheria.
Mhe.Katimba amesema kuwa  Wanawake, watoto na watu wenye mahitaji maalum ndio walengwa kwenye kampeni hiyo na wameandaa program maalum kufikia watoto shuleni ili kupata elimu ya kujilinda na ukatili.
” Tunaandaa kanzi data ya mawakili ambao wako ndani ya UWT Ili kuwa na timu kubwa ya watu watakao toa msaada kisheria kwa wananchi katika Mikoa waliyopo,”amesema Mhe.Katimba
Aidha amefafanua  kuwa Rais Dk.Samia  aliona  wananchi wanahitaji msaada ndio maana alianzisha kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia ambayo imekuwa na matokeo chanya
Katika hatua nyingine amesema  kupitia kampeni hiyo  wametengeneza programu ya kuwafikia watoto na kuwajengea uelewa namna ya kuepuka vitendo vya ukatili.
“Kutakuwa na programu maalumu ambayo itaaenda kuwafikia watoto na kutoa uelewa namna wanavyoweza kuepuka na vitendo vya ukatili,”amesema
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga ,amesema kuwa uzinduzi wa Kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka kukiwa na matukio mengi yasiyofaa  katika jamii.
“Kampeni hii imekuja wakati mwafaka  kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza na tunaamini itakuwa muarobaini wa matukio,”amesem
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Sheria ya UWT, Zainab Katimba ,akielezea malengo ya kampeni hiyo wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Bi.Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septe.ba 7,2024 jijini Dodoma.

MBUNGE  wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mhe.Subira Mgalu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septe.ba 7,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizindua  kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor