Na Gideon Gregory, Dodoma.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imesema mauaji ambayo yameendelea kushika kasi licha ta jeshi la polisi kufanya jitihada za kuwakamata watahumiwa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria imeweza kubaini visababishi mbalimbali ikiwemo ulipaji kisasi na imani za kishirikina.
Hayo yameelezwa leo Agosti 30,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kulaani wimbi la mauaji nchini.
“Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha kunakuwepo na taratibu za kuimarisha ulinzi wa usalama wa raia, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema katika kushughulikia matukio ya uhalifu kwa kushirikiana na Mamlaka husika,
Jaji Mwaimu amesema wananchi pia wajenge utamaduni wa kuheshimu sheria za nchi na haki za binadamu, watambue namna bora ya kupata suluhu ya migogoro inayowakabili katika ngazi zote za jamii, na kushughulikia migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kujichukulia sheria mikononi.
Pia Jaji Mwaimu amesema, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari waendelee kutoa elimu kwa umma kuhusu taratibu zilizopo za namna ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii kupitia sheria, na hivyo kulinda haki za binadamu na utu wa mtu.
Jaji Mwaimu amesema Matukio hayo ya mauaji yamekuwa yakiripotiwa na vyanzo mbalimbali vya taarifa hususani vyombo vya habari na taarifa kutoka jeshi la polisi nchini.
“Mara kadhaa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassa amekua akilaani na kukemea vitendo hivyo vya mauaji na sisi kama Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengine wameshiriki katika mijadala kupitia vyombo vya habari”amesema Jaji Mwaimu
Hata hivyo katika ufuatiliaji wake THBUB imeweza kubaini mambo kadhaa ikiwemo tabia ya baadhi ya wananchi kutokuzingatia sheria za nchi na kujichukulua sheria mikononi.