Featured Kitaifa

WADAU WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAONO YAKE MASHIRIKA KUWEKEZA NJE

Written by mzalendoeditor

 

ARUSHA.

Wadau wanaoshiriki katika Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, Jijini Arusha, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa na shahuku ya kuona Mashirika ya Umma yanaimarika kiutendaji na kutimiza hazma ya kufanya Biashara nje ya mipaka ya Tanzania.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano maalum unaojadili namna mashirika ya umma yataweza kuwekeza na kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania ulioandaliwa na Benki ya CRDB ambao walitoa washilisho kuelezea uzoefu wao kama Taasisi ya Kitanzania inayotoa huduma zake ya mipaka ya nchi.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa Habari, Mtendaji Mkuu wa Mbasi yaendayo kwa haraka, DART, Dkt. Athumani  Kiamia, amesema mkutano huo umetoa fursa kwa viongozi kupata uzoefu kutoa katika Benki hiyo ambao wamefanikiwa kutoka nje, nakwamba wameona kwa kufanya hivyo kunakuwa na wigo mpana wa kuendeleza Biashara na kuimarisha uchumi wan chi.

“Mchango wa hizi Taasisi kama CRDB na nyingine kuanza kuwekeza nje na maana nyingi sana, kwanza wataalamu wetu mbalimbali watakwenda kufanya kazi kule, lakini  soko linaongezaka kutokana na taasisi zinakuza mitaji yao na kupelekea kuongeza huduma zake katika maeneo mengine.

“Hatua hii inaifanya nchi yetu iweze kujiimarisha zaidi kidiplomasia. Jambo hili ni la kupongezwa sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan  kwa kubuni jambo hili kwamba mashirika sasa yajitanue“ amesema Dkt. Kiamia.

Akizungumza akipokuwa akitoa wasilisho kuhusu uzoefu na mafanikio waliyoyapata katika huduma wanazotoa nje ya nchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa uwekezaji huo umeleta mafanikio katika uchumi wa Tanzania, pamoja na kusaidia kujenga uwezo wa kiuchumi katika nchi waliyowekeza, na kuiwezesha Sekta Binafsi kufanya malipo ya Biashara zao katika nchi zote mbili.

“Tunaamini wadau waliopo katika mkutano huu wana malengo ya kuwekeza na sisi kwa uzoefu wetu muda wote tunaamini katika ushirikiano, hivyo kikao cha leo kimetoa mwanga na tutaendelea kutoa ushirikiano kwa siku zinazoendelea“ amesema Nsekela.  

About the author

mzalendoeditor