Featured Kitaifa

NIT YATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa kituo cha kikandacha umahili katika Usalama barabarani NIT Bw. Godlisten Msumanje akizungumza mara baada ya kutoa elimu katika shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma.

……

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia kituo chake cha Umahiri cha Kikanda Katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani kimetoa Mafunzo ya Usalama Barabarani Mkoani Dodoma.

Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 28.8.2024 na 29.8.2024 wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kumi na moja(11) ikiwemo shule ya msingi Mazengo ,Kikuyu,Amani,Mlezi, Mlimani, Makole, Kizota, Chadulu, Mlimwa, na Kisasa.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wanafunzi hao uwelewa wa matumizi sahihi ya barabara.

Akizungumza mara baada ya kutoa elimu Mkuu wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda Katika Usalama Barabarani NIT Ndg. Godlisten Msumanje amesema katika elimu waliyoitoa ni kwaajili ya kujenga uelewa na ufahamu kwa wanafunzi ambao bado ni wadogo ili wajue matumizi sahihi ya barabara na kuwabadilisha tabia ya watumiaji wa barabara.

“Lengo ni kuwajengea uelewa na ufahamu wanafunzi wa shule za msingi katika matumizi sahihi ya barabara ikiwemo aina za vivuko, namna ya kuvuka na kutembea barabarani wakiwa salama”amesema.

Amesema kuwa jukumu la usalama barabarani ni la watu wote na kutoa wito kwa jamii yote kufuata sheria zote za usalama barabarani na kuwakumbusha madereva wote kuwa makini wawapo barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Insp. Saburi Chutto ametoa wito kwa madereva wote wa serikali, mabasi ya abiria, bodaboda kutii sheria za usalama barabarani na kufuata ishara na michoro kinyume na hapo watapewa adhabu.

“Hivyo niwaase wote kuzingatia usalama wa watumiaji wote wa barabara ili kuweza kuepuka ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kughalimu maisha ya watu na wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu”, amesema.

Sambamba na hilo amebainisha hasara za kutokuheshimu alama za barabarani kuwa ni kusababisha ajali na kuwaachia ulemavu watu pamoja na kusababisha hasara kwa taifa kwa kuharibu miundombinu ya barabara.

Mkuu wa kituo cha kikandacha umahili katika Usalama barabarani NIT Bw. Godlisten Msumanje akizungumza mara baada ya kutoa elimu katika shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma.

Sajenti wa polisi Asha Abdul kutoka makao makuu ya kikosi cha Usalama barabarani makao makuu Dar es Salaam Dawati la elimu kwa umma akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Jijini Dodoma.

Mkaguzi msaidizi wa polisi Insp. Saburi Chutto akizungumza mara baada ya zoezi la kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Jijini Dodoma kukamilika.

Sajenti wa polisi Asha Abdul kutoka makao makuu ya kikosi cha Usalama barabarani makao makuu Dar es Salaam Dawati la elimu kwa umma  akitoa vifaa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda Katika Usalama Barabarani NIT Bw.Godlisten Msumanje akikabidhi zawadi na vifaa kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru iliyopo Jijini Dodoma.

Picha ya pamoja kati ya watumishi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), maafisa kutoka jeshi la polisi na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor