Featured Kitaifa

WANANCHI WA MLIMBA WAMSHUKURU MHE. SAMIA KUWAFIKISHIA ELIMU YA FEDHA

Written by mzalendo
Diwani wa Kata ya Ching’anda katika Halmashauri ya Mlimba Mhe. Hassan Kidapa akizungumza na wananchi waliohudhuria program maalum ya elimu ya fedha illiyotolewa na Wizara a Fedha katika Halmashauri ya Mlimba.
Diwani wa Kata ya Mlimba, Halmashauri ya Mlimba Mhe. Waraji Hassan akifafanua jambo kwa wananchi wa Mlimba waliohudhuria program maalum ya elimu ya fedha illiyotolewa na Wizara a Fedha katika Halmashauri ya Mlimba.
Baadhi ya wananchi kutoka katika kata saba (7) za Halmashauri ya Mlimba wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani) katika program ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha.
Mshiriki wa program ya elimu ya fedha kwa umma kutoka Kata ya Mlimba, Halmashauri ya Mlimba, Bw. Cosmas Mfilinge akichangia jambo katika program ya elimu ya fedha iliyotolewa katika Halmashauri hiyo.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Mlimba wakati wa program maalum ya elimu ya Fedha iliyotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha nchini katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Wizara ya Fedha – Morogoro)
Na. Ramadhani Kissimba, WF, Morogoro
 
Wananchi wa Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka na kuwafikishia elimu ya fedha ambayo itawasaidia wananchi waishio vijijini kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ya fedha yakiwemo ya uwekezaji na mikopo.
 
Akizungumza katika mfufulizo wa program ya elimu ya fedha kwa umma inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikia na washirika wa sekta ya fedha nchini, Diwani wa kata ya Ching’anda katika Halmashauri ya Mlimba Mhe. Hassan Kidapa amesema kupitia elimu iliyotolewa wananchi watakwenda kunufaika hasa katika kupanga mipango na kuitumia vizuri.
 
‘’Kwa kipindi hiki ambacho nimesikiliza elimu hii ni Dhahiri kuwa wananchi wengi wanakwenda kunufaika, watanufaika kwanza kwa kuweza kupanga mipango na kuitumia vizuri kwa kadiri mipango yao walivyoipanga na pili kwa kutumia vizuri Taasisi za fedha zilizopo Wilayani Mlimba’’. Alisema Mhe. Kidapa.
 
Mhe. Kidapa aliongeza kuwa wananchi wakishikamana vizuri na Taasisi za fedha kwa kufuata miongozo na taratibu za fedha maana yake wananchi watapata ajira na faida kubwa sana kwa kuwekeza kile kiasi kidogo walichonanacho kwenye Taasisi za fedha.
 
Aidha, Mhe. Kidapa alisema awali kabla ya elimu hiyo kutolewa, wananchi wa Mlimba wanapata pesa nyingi lakini zinazitumia kinyume na mpangalio na hivyo ni mategemeo yake kuwa baada ya elimu hii wale waliokuwa wanatumia fedha hovyo au kukopa kupitia mikopo umiza wataacha kufanya hivyo.
 
Aliiomba Serikali kuendelea kutoa semina za namna hiyo hasa kwa ngazi za vijijini ili wananchi waweze kuona faida na waweze kuchangia kipato cha nchi na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Awali mtoa huduma ndogo za fedha kutoka Karoli Microcredid Company (T) Limited iliyopo Halmashauri ya Mlimba, Bw. Baraka Kagoma alisema wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na wananchi wengi kukopa bila kujua mkopo huo ataufanyia nini na  kushindwa kufanya marejesho kama ilivyotarajiwa, hivyo ujio wa elimu hiyo itawasaidia kupunguza changamoto hizo kwa wakopati na Taasisi zao kujiendesha kwa faida.
 
Program ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Mlimba ililenga kuwawezesha wananchi kupata maarifa kuhusu namna bora ya kusimamia rasilimali fedha na ilishirikisha wananchi kutoka katika kata saba (7) za Chita, Ching’anda, Chisano, Kalengakelo, Mlimba, Utengule, Kamwena na Masagati.

About the author

mzalendo