Featured Michezo

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI UBINGWA KWA MSHINDI WA KIZIMKAZI SAMIA CUP 2024- ZANZIBAR

Written by mzalendo

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi Kombe kwa Mabingwa wa Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 ambayo ni timu ya Shule ya Sekondari Kusini mara baada ya kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0 katika mchezo wa fainali uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar tarehe 24 Agosti 2024 ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifuatilia mchezo wa mpira wa miguu fainali ya Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 baina ya Shule ya Sekondari ya Kusini na Shule ya Sekondari Muyuni uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar tarehe 24 Agosti 2024 ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi.

About the author

mzalendo