Naibu Waziri Ofisi Ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deus Sangu akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Wa Umma katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo jijini Dodoma Agosti 23 mara baada ya kufanya Ziara fupi ya kikazi Ofisini hapo.
Naibu Waziri Ofisi Ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deus Sangu akiasalimiana na Viongozi wa Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Wa Umma baada ya kufika katika Sekretarieti hiyo jijini Dodoma Agosti 23 kwa Ziara fupi ya kikazi.
Naibu Waziri Ofisi Ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deus Sangu(katikati), akiwa katika picha ya pamoja ya Viongozi pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Wa Umma jijini Dodoma Agosti 23 baada ya kufanya Ziara fupi ya kikazi ofisini hapo.
……
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Clement Sangu amesema suala la maadili ndiyo silaha na kila kitu katika jamii na kwamba maadili ni suala mtambuka ambalo linatakiwa kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye utumishi wa umma.
Mhe. Waziri amesema hayo alipotembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu jijini Dodoma tarehe 23 Agosti, 2024 ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ofisi hizo tangu ateuliwe kushika wadhifa wa Naibu Waziri.
“Maadili ni tuzo kubwa katika Taifa letu, ndio maana kila mahali unapopita, maadili yanapewa kipaumbele kwasababu ni jambo mtambuka,” alisema.
Mhe. Sangu katika hotuba yake ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kufanya kazi kwa weledi na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya maadili.
Ameitaja misingi hiyo kuwa ni kuzingatia utaalam, kuwa mwadilifu na kutimiza wajibu.
“Misingi hii isipozingatiwa usababisha uvunjifu wa sheria, mienendo isiyofaa na utovu wa nidhamuazi,” amesema.
Aidha, Mhe. Sangu ametoa rai kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutumia mbinu za kisasa katika utendaji wake wa kazi hasa zoezi ila uhakiki wa mali na madeni ya viongozi.
“Tumieni mbinu za kisasa za kiuchunguzi mnapo hakiki mali za viongozi katika kufuatilia vitendo vya ukiukwaji wa Maadili kwa viongozi wa umma. Hili zoezi linaweza kufanyika vizuri kwa kutumia TEHAMA.”
Katika hatua nyingine, Mhe. Sangu amesema, kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ujazaji wa matamko kwa njia ya mtandao (On line Decrelation Systerm) kutasaidia kupata ukweli na uhalisia wa matamko ya viongozi wa umma kwa urahisi na usahihi na kuondokana na mzigo uliokuwepo wa mlundikano wa makaratasi kama ilivyokuwa hapo awali na kwamba suala hili liwe endelevu na lipewe kipaumbele kwa uzito wake.
“Pamoja na mfumo huu, fanyani utafiti kuhusu hali ya maadili nchini na kuwachukulia hatua viongozi wote wanaokiuka maadili ikiwemo wanaotoa matamko ya uongo. Hawa wapelekeni kwenye Baraza la Maadili,” alisema.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Bw. Waziri Kipacha aliyataja majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa ni pamoja na Kupokea matamko ya raslimali na madeni, Kupokea malalamiko kuhusu ukiukwaji wa maadili kutoka kwa wananchi, Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma au malalamiko dhidi ya kiongozi, Kufanya uhakiki wa raslimali na madeni ya viongozi wa Umma, Kutoa elimu ya maadili kwa viongozi wa umma, Kufanya utafiti kuhusu hali ya maadili nchini na Kubuni mikakati ya kukuza uadilifu nchini.
Kikao hicho kilichojumuisha watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili Makao Makuu na ofisi ya Kanda ya Kati, kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.