Featured Kitaifa

SHERIA KUTUNGWA PASIPO KUZINGATIA TAFITI CHANZO CHA KUFANYIWA MAREKEBISHO MARA KWA MARA- DKT. RWEZIMULA

Written by mzalendo

 

NAIBU  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza wakati akifungua  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Jaji wa Mahakama ya Rufani,Winifrida Korosso,akizungumza wakati wa Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw.George Mandepo ,akizungumza wakati wa  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi, iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,(hayupo pichani)  wakati akifungua  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akizindua The Law Reformer yenye lengo la kutengeneza Jukwa la fursa kwa watu mbalimbali kujadiliana na kutoa maoni kuhusu masuala muhimu ya Kitaifa na Kimataifa mara baada ya kufungua  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akimkabidhi Vitendea kazi Mwenyekiti  wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Jaji wa Mahakama ya Rufani,Winifrida Korosso,mara baada ya kuzindua The Law Reformer yenye lengo la kutengeneza Jukwa la fursa kwa watu mbalimbali kujadiliana na kutoa maoni kuhusu masuala muhimu ya Kitaifa na Kimataifa  baada ya kufungua  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akionyesha Vitabu mara baada ya kuzindua The Law Reformer yenye lengo la kutengeneza Jukwa la fursa kwa watu mbalimbali kujadiliana na kutoa maoni kuhusu masuala muhimu ya Kitaifa na Kimataifa  baada ya kufungua  Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

NAIBU  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua   Warsha Juu ya Umuhimu wa Utafiti katika Maboresho ya Sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi iliyofanyika leo Agosti 21,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
IMEELEZWA  kutokana na Sheria kutungwa pasipo kuzingatia tafiti imelazimika kwa baadhi ya Sheria kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara na nyingine kukosa umuhimu mara tu baada ya kutungwa kwake.
Hayo yameelezwa leo Agosti 21,2024 Jijini Dodoma na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Flanklin Rwezimula wakati akifungua warsha kuhusu juu ya umuhimu wa utafiti katika maboresho ya sheria Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi 
Dkt.Rwezimula amesema kuwa kushindwa kuhusisha utafiti wa kina katika utungwaji wa sheria, pengine imekuwa vigumu kuelezea Bungeni madhumuni na sababu za kitaalamu za utungwaji au urekebishwaji wa baadhi ya sheria na hivyo, zoezi la kupitishwa sheria kuchelewa au kukosa msukumo ndani ya Bunge letu.
 
“Sheria zinapotungwa zinalengwa kwa ajili ya jamii ambayo inaathirika na hali fulani ya kiuchumi,kijamii au kisiasa,Serikali kupitia mapendekezo ya Tume ya Mhe.Msekwa ilitarajia kuwa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania itumike ipasavyo katika kila hatua za utungwaji au maboresho ya Sheria”amesema Dkt.Rwezimula
Aidha  ametoa rai kwa Wizara na taasisi za Serikali kuzingatia mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na Tume ya Haki jinai kwa Serikali yatekelezwe kwani utekelezaji utaleta tija kubwa kwa sheria zinazotungwa na Bunge. 
“Niwaagize sasa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania kwa kushirikiana na Mwanasheria mkuu wa Serikali kuweka utaratibu mzuri ambao utawezesha wadau kushirikishwa kwa karibu sana katika hatua zote za utungwaji sheria”amesema. 
 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Tabia Tanzania Jaji wa Mahakama ya Rufani Winfrida Karosso amesema kuwa Tume ya kurekebisha sheria nchini ni chombo mahsusi kilichoundwa kwa lengo la kupitia sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuzifanya ziendane na wakati kwa maendeleo endelevu ya taifa.
“Niwazi kuwa ili tume iweze kutimiza jukumu hili kwa ufanisi ni lazima ishirikiane na wadau wote ili kupata maoni yatakayowezesha kutoa mapendekezo ya maboresho”, amesema. 
Aidha ametoa rai kwa Tume kuhakikisha inatumia kila njia kuhakikisha inawavutia na kuwafikia wananchi wengi ambao mwisho wa siku ndio watumiaji wa sheria hizo ili waweze kutia maoni ya marekebisho na maboresho ya sheria. 
“Endapo wananchi watapatiwa elimu ya kutisha na kushiriki kutoa maoni, sina shaka yoyote kuwa utekelezaji wa sheria utakuwa rahisi a hautakuwa na upinzani kutokana na mchakato wa maboresho kuwa shirikishi kabla ya kutungwa au kutekebishwa kwa sheria husika”,amesema.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Bw.George Mandepo amesema lengo la warsha hiyo ni kujadili umuhimu wa tafiti katika utungaji wa marekebisho ya sheria na kubainisha umuhimu wa tafiti katika maboresho ya sheria nchini. 
“Utafiti wakati wa kutunga sheria ni jambo muhimu sana kwa kuwa unawezesha vyombo vya maamuzi kuwa taarifa za kutosha na ufahamu wa eneo linalotungiwa sheria”amesema. 
Pia emeongeza kuwa mesema Tume ya kurekebisha sheria Tanzania ilianzishwa na sheria ya tume sura 171 ambapo ilianza rasmi Oktoba 21,1983 ikiwa na majukumu makuu matatu ikiwa ni kufanya mapitio ya sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa mapendekezo ya kurekebisha sheria hizo ili ziakisi mabadiliko tanayotokea katika jamii katika nyanja za kisiasa.

About the author

mzalendo