Featured Kitaifa

AMREF TANZANIA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI – DODOMA

Written by mzalendo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunga maadhimisho ya siku ya vijana kitaifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.
Mbali na mambo mengine, Waziri Ridhiwani Kikwete ametembelea banda la Amref Tanzania na kuelezwa namna AmrefTanzania inavyounga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika kwa kushirikiana na wadau wake inavyolenga kutatua changamoto zinazowakabili (vijana) katika masuala ya Afya ili kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni; “Vijana na Matumizi ya Fursa za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu”.

About the author

mzalendo