BENKI ya Maendeleo (TIB) imesema katika kuwasaidia wakulima kwa kutoa mikopo ya kilimo ili kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika uzalishaji.
Mtumishi wa Benki ya TIB Monica Mzilu amwyaswma hayo wakati akizungumza kwenye maonesho ya wakulima ,wafugaji na wavuvi yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema ,benki hiyo ina mfuko unaotoa mikopo inayotolewa kwa wakulima kuanzia shilingi milioni 50 hadi bilioni 2 kwa makampuni kwa riba ya asilimia tano na vikundi vilivyosajiliwa kama saccos au ‘association’ kuanzia milioni 50 mpaka bilioni moja kwa riba ya asilimi nne tu ili waweze kukopesha kwa wakulima wadogo kwa riba isiyozidi asilimia nane.
“Tunatoa mikopo hiyo yote kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo yaan kuanzia mwanzo hadi kwenye masoko ,kwa maana kwamba tunatoa mkopo kujenga maghala au kununua vifungashio au kama mtu anataka kuchakata mazao ili kuongeza thamani ili mradi wazo husika likidhi vigezo .”
Amesema,wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima luhusu fursa zilizopo benki hiyo katika maeneo tofauti ikiwemo katika maonesho ya sabasaba na Nanenane .
Kwa mujibu wa Mzilu pia wamekuwa wakiwatembelea wakulima na kuwaelimisha wafahamu wanachokitaka lakini pia wanawaelimisha jinsi ya kutunza fedha.
Aidha amesema benki hiyo ina ofisi katika kanda nne zilizopo kwa sasa ni Kanda Kanda ya Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na Arusha
Xxxx