Featured Kitaifa

HATUNA DENI NA MTATURU

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema serikali imeridhia kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni 104 kwa ajili ya kujenga madarasa matatu na matundu 6 ya vyoo ili kukamilisha shule Shikizi iliyopo Kijiji cha Sambaru na hivyo kuiwezesha kuanza kupokea wanafunzi January 2025.

Mtaturu amesema hayo Agosti 4,2024,akiwa katika muendelezo wa ziara yake jimboni ambapo ametembelea kitongoji cha Kipompo Kijiji cha Sambaru.

“Katika ujenzi wa shule hii shikizi wananchi wamejitolea kujenga madarasa manne na mimi niliwapelekea Shilingi Milioni 8 wamepaua na sasa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ametuletea Shilingi Milioni 104 ili wajenge madarasa mengine na shule ifunguliwe Januari 2025,hakika upendo wa Rais kwetu ni mkubwa sana sana,”amesema Mtaturu.

Ujenzi wa shule hiyo shikizi ulianza mwaka 2021 kwa kufanya changizo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge Miraji
Mtaturu na kufanikiwa kujenga madarasa manne na nyumba ya walimu ambapo Mbunge Mtaturu aliwachangia Shilingi Milioni 8 iliyofanikisha kupaua madarsa manne yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Baada ya hapo Mbunge Mtaturu alipeleka maombi Wizara ya TAMISEMI wapatiwe fedha za kuongeza madarasa ili shule ikamilike na ianze kuondoa changamoto ya watoto kutembea Kilomita 12 kuelekea Shule ya mama ya Msingi Sambaru.

Diwani wa Kata ya Mang’onyi Innocent Makomelo amemshukuru Mbunge kwa kuwasemea bungeni na hatimaye Kata ya Mang’onyi imepata fedha nyingi za miradi ya Elimu,Afya,Miundombinu ya Umeme,Maji na Barabara ikiwemo barabara muhimu ya Misughaa-Msule-Kipompo.

Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mang’onyi Hussein Dede amemshukuru kwa kazi na msaada alioutoa katika Kitongoji cha Kipompo kupitia mradi huo wa shule na kusema hawana deni nae na 2025 ataendelea kuwa Mbunge wao.

About the author

mzalendoeditor