Featured Kitaifa

BENKI YA TAIFA YA USHIRIKA KUZINDULIWA SEPTEMBA MWAKA HUU

Written by mzalendo

 

MRAJIS  Msaidizi Sehemu ya uhamasishaji na uratibu Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Ibrahim Kadudu,akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima Nanenane  yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

MRAJIS  Msaidizi Sehemu ya uhamasishaji na uratibu Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Ibrahim Kadudu,akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima Nanenane  yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MRAJIS  Msaidizi Sehemu ya uhamasishaji na uratibu Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Ibrahim Kadudu, amesema benki ya Taifa ya Ushirika itazinduliwa mwezi Septemba mwaka huu.

Kadudu, ameyasema hayo leo Agosti 5,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima Nanenane  yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

“Mwenyezi Mungu akijalia kwa mwezi wa tisa ambao tunakwenda benki ya taifa ya ushirika itakuja kuzinduliwa rasmi ambayo itakuwa na matawi makuu matatu.

Bw.Kadudu amesema  kwa kuanzia matawi hayo yatakuwa katika mikoa wa Kilimanjaro, Dodoma pamoja na Mtwara.

“Kwa makao makuu yenyewe wanaushirikia walikubaliana kwamba yawe jijini Dodoma”amesema

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa Tume hiyo kwenye maonesho ya wakulima mwaka huu amesema mwaka huu wameratibu kijiji cha ushirika katika viwanja hivyo vya Nanenane.

“Sisi kama waratibu wa shughuli za ushirika mwaka huu tumeratibu kijiji cha ushirika na lengo likiwa kuunganisha wanaushirika katika maeneo yao mbalimbali ambayo wanayafanyia kazi kuja kuwaonyesha shughuli zao wanazozifanya”amesema

Amesema , pia katika kijiji hicho vipo vyama mbalimbali ambavyo wameshirikiana navyo katika maonyesho hayo ya wakulima nanenane.

“Lakini katika kijijii chetu tunao wadau wetu wa kuongeza huduma kwenye vyama zile huduma za elimu huduma za mafunzo, sambamba na huduma za uongezaji thamani kwenye shuguli za vyama vya ushirika”alisema

Hata hivyo, amesema kuwa katika kijiji cha ushirika mwaka huu kuna takribani wadu 21 ambao wameungana katika maonosho hayo.

About the author

mzalendo