Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametembelea Banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mhe. Mkuu wa mkoa alielezwa Majukumu ya THBUB ikiwemo kuhamasisha jamii huhusu hifadhi ya haki za binadamu na utawala bora nchini, kupokea malalamiko na kufanya uchunguzi ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.
Mhe. Senyamule ameipongeza THBUB kwa kazi nzuri ya kukuza na kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini
Hata hivyo, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa THBUB kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii ili kupunguza matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora katika jamii.