Featured Makala

HIZI NDO SIFA ZINAZOTAKIWA KWA KIONGOZI TLS

Written by mzalendoeditor

Wagombea wa nafasi ya Urais katika Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) wakiwa kwenye mdahalo

Na Mwandishi Wetu

JOTO la uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) limeendelea kupanda kwa wagombea huku wadau wakiwa na maoni tofauti tofauti kwenye midahalo mitandaoni kiongozi anayetakiwa ngazi ya urais TLS.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 2, 2024 ambapo wagombea sita wamejitosa kuwania nafasi ya urais.

Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni Wakili Sweetbert Nkuba, Paul Kaunda, Revocatus Kuuli, Emmanuel Muga, Ibrahim Bendera na Boniface Mwabukusi.

Katika mdahalo wenye mada isemayo umuhimu na changamoto za TLS katika kusimamia sheria na haki nchini, kwenye kundi songozi la Katiba ya watu wa Tanzania, mmoja wa wachangiaji Glory Mathew amesema ujasiri ni sifa muhimu, lakini sio ya pekee inayohitajika kwa kiongozi wa TLS kwa kuwa ili kuwa uongozi bora na wenye tija, kiongozi wa TLS anapaswa kuwa na sifa zaidi ya ujasiri.

Amesema kiongozi anapaswa kuzingatia uadilifu na maadili kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha anafanya maamuzi kwa misingi ya haki na ukweli.

Pia amesema ujuzi wa kitaaluma:Lazima awe na uelewa wa kina wa sheria na uwezo wa kutafsiri sheria kwa usahihi. Hii inasaidia katika kutoa ushauri sahihi na kuongoza chama kwa misingi ya kitaaluma.

“Uwezo wa Kuongoza na Kusimamia: Kiongozi wa TLS anahitaji kuwa na uwezo wa kuongoza na kusimamia watu na miradi mbalimbali. Hii inajumuisha kuwa na uwezo wa kupanga, kuamua, na kutekeleza mipango kwa ufanisi,”amesema.

Kadhalika, anasema sifa nyingine awe na uwezo wa kuwasiliana:

Lazima awe na uwezo bora wa kuwasiliana kwa njia mbalimbali. Hii ni pamoja na kuandika vizuri, kuzungumza kwa ufasaha, na kusikiliza kwa makini.

“Uwezo wa Kushirikiana:

Kiongozi mzuri anapaswa kuwa na uwezo wa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo wanachama wa TLS, serikali, na mashirika mengine. Hii inajumuisha kuwa na uwezo wa kujenga mahusiano mazuri na kushirikisha wengine katika maamuzi,”amesema.

Pamoja na hayo, amesema awe na uwezo wa kutatua migogoro:

Lazima awe na uwezo wa kutatua migogoro kwa njia ya amani na kwa haraka. Hii inasaidia katika kudumisha utulivu na umoja ndani ya chama.

“Awe na mtazamo wa kimkakati:

Kiongozi wa TLS anapaswa kuwa na mtazamo wa kimkakati, akijua malengo ya muda mrefu na jinsi ya kuyafikia. Hii inajumuisha kuweka mipango ya maendeleo na kuhakikisha kuwa chama kinaendelea mbele,”amesema.

Amesema suala la uwazi na uwajibikaji ni muhimu kwa kiongozi TLS anapaswa kuwa muwazi na muwajibikaji wazi na wawajibikaji katika maamuzi na vitendo vyake. Hii inasaidia kujenga imani na uaminifu kati yake na wanachama wa TLS na jamii kwa ujumla.

“Kiongozi wa TLS anapaswa kujitolea na awe na bidi kwa ajili ya maendeleo ya chama na taifa kwa ujumla.Ingawa ujasiri ni sifa muhimu kwa kiongozi yeyote, kiongozi wa TLS anapaswa kuwa na mchanganyiko wa sifa nyingi zaidi,”amesema.

KUONGEZWA MUDA WA UONGOZI

Katika mjadala huo, wachangiaji wengi waliunga mkono hoja ya kuongezwa muda wa urais wa TLS kutoka mwaka mmoja na kuwa mitatu kwa kuwa inasaidia kujenga taasisi imara.

Mmoja wa wachangiaji, amesema kukaa kwenye kiti hicho ni hoja mama kabisa ni dhahiri mabadiliko yoyote yanahitaji muda na pia muda wa mwaka mmoja si kipimo sahihi sana kwa utendaji kazi.

Hata hivyo, mmoja wa wachangiaji ametofautiana na wengine akidai kuwa taasisi ya TLS inaushawishi mkubwa kwenye mambo ya kisiasa hivyo kumuweka kiongozi kukaa muda zaidi yam waka mmoja kunaweza kusababisha akajichimbia na kutengeneza mizizi hatimaye kutumiwa kisiasa.

“Yanatakiwa mabadiliko makubwa ya Sheria iliyounda TLS au sheria hiyo ifutwe na TLS iwe chama kama vyama vingine kama Chama cha Walimu, Chama wafanyakazi wa ndani, Chama cha Madaktari nk.Hakutakuwa na shida tena kuhusu muda wa Rais wa TLS kuwepo madarakani, maana itaandikwa kwenye katiba yao,”amesema.

About the author

mzalendoeditor