Featured Kitaifa

DKT. TULIA NA RAIS PUTIN WAJADILIANA NAMNA BORA YA KUIMARISHA AMANI DUNIANI

Written by mzalendo

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 12 Julai, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.

Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”

About the author

mzalendo