Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Bina ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa kazi nzuri ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini.
Bina ameyasema hayo leo Julai 09, 2024 alipotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam ‘ Sabasaba ‘ yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
“Kazi yenu ni nzuri sana, mnafanya kazi kubwa ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini, niwapongeze Taasisi zote zilizopo chini ya Wizara kuanzia Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).