Featured Kitaifa

MJUMBE HALIMASHAURI KUU YA CCM SONGWE ATOA VIFAA VYA OFISI KWA JESHI LA POLISI

Written by mzalendo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga amepokea Komputa 02 Mpakato (Laptop) zilizotolewa kwa lengo la kusaidia shughuli za Jeshi la Polisi mkoani Songwe.

Vifaa hivyo vimetolewa Julai 05, 2024 na mdau wa Jeshi la Polisi Mh. Ombeni Nanyaro ambaye ni Mjumbe Halimashauri Kuu ya Ccm Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kutunzia nyaraka mbalimbali za ofisi.

Kamanda Senga amemshukuru Mh. Nanyaro kwa msaada alioutoa na amemuomba kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika harakati za kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya uhalifu na wahalifu ili jamii iendelee kuwa salama kwa manufaa na maendeleo ya nchi yetu.

About the author

mzalendo