Featured Kitaifa

DKT. YONAZI AKOSHWA NA KOZI YA USALAMA WA MTANDAO VYUO VYA WIZARA YA FEDHA

Written by mzalendo

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Sehemu ya Uendelezaji wa Wanafunzi Kitaaluma na Kitaalamu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Bw. Imani Matonya, kuhusu programu za Chuo hicho, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.

Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, amevipongeza Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Fedha kwa kuwa na programu zinazoendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Dkt. Yonazi, alitoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo Vyuo hivyo kikiwemo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanzisha Kozi ya Usalama Mtandaoni (Cyber Security)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, akiagana na Afisa Habari Mwandamizi kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amevipongeza vyuo kwa kuanzisha kozi mpya ya Usalama wa Mtandao (Cyber Security).

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Sehemu ya Uendelezaji wa Wanafunzi Kitaaluma na Kitaalamu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Bw. Imani Matonya, kuhusu programu za Chuo hicho, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Bw. Bashiru Taratibu, akitoa maelezo ya umuhimu wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ambapo inasaidia kupunguza shinikizo kwa bajeti kuu ya Serikali wakati wa utekelezaji wa miradi, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Emmanuel Kellya (kulia), akitoa maelezo ya Mfumo wa Manunuzi wa NeST kwa wakazi wa Dar es Salaam waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

About the author

mzalendo