Featured Kitaifa

WANANCHI WA KAHAMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA ELIMU YA FEDHA KWA UMMA

Written by mzalendo

 

Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Bw. Masoud Kidetu, Nyenzo ya kufundishia elimu ya fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu hiyo katika maeneo yake ya kazi, mara baada ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha, kufika katika Halmashauri ya Manispasa hiyo kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na wananchi waliyofika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Bw. Masoud Kidetu (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha. Wa pili kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, wa kwanza kushoto ni Afisa Biashara na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Mkoa wa Shinyanga Bi. Rose Tungu, wa kwanza kulia ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Norasco Mbawala.

Baadhi ya wajasiriamali na wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga  bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha (Vikoba) na kuhifadhi fedha za vikundi hivyo  benki, utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kuhusu masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima za biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha ili kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.

Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akitoa elimu ya fedha kwa baadhi ya waananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, kabla ya kuweka filamu ya elimu ya fedha ili wananchi hao waweze kujifunza kwa njia ya burudani, ambapo washiriki wengi wa mafunzo hayo waliipongeza Wizara ya Fedha kwa kutumia njia hiyo ya  mafunzo ya elimu ya fedha kwa kudai kuwa haichoshi na ina mafunzo mengi kwa sababu imebeba uhalisia wa maisha ya wananchi wengi.

Afisa Biashara na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha mkoa wa Shinyanga Bi. Rose Tungu akizungumza na washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama (hawapo pichani), wakati wa mafunzo hayo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, mafunzo hayo yalihudhuriwa na makundi mbalimbali ikiwemo, watu wenye mahitaji maalum, wafanyabiashara, wajasiriamali, bodaboda, watoa huduma ndogo za fedha, na wananchi ambao ni watumiaji wa huduma za fedha ambapo walipata fursa ya kupata elimu kuhusu uwekaji  wa akiba, uwekezaji, utunzaji wa fedha binafsi, matumizi sahihi ya fedha na namna bora ya kuandaa maisha ya uzeeni na kustaafu.

Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Mwile Kauzeni, akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi za huduma za fedha zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na namna ya kuzitambua taasisi hizo ili  wananchi wanapotaka kukopa waweze kuepuka kukopa fedha katika taasisi zisizo rasmi, kuepuka mikopo umiza baada ya baadhi ya  washiriki hao wa mafunzo ya elimu ya fedha kutaka kufahamu wanawezaje kujua kwamba taasisi wanazotaka kukopa fedha zimesajiliwa.

Picha za matukio mbali mbali ya mafunzo ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, elimu hiyo ya fedha ilianza kutolewa maeneo ya mijini kupitia maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kwa Mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza na Arusha, ambapo kwa sasa programu hiyo imejikita kuwafikia wananchi wote kwa lengo la kuwaongezea uelewa wa masuala ya fedha ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika mahitaji na matumizi ya huduma za fedha, maeneo mengine yaliyofikiwa ni pamoja na Mkoa wa Manyara, Singida, Kagera, Rukwa, Kigoma, Tabora, Simiyu na Shinyanga.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha-Shinyanga)

About the author

mzalendo