Featured Kitaifa

DKT.NCHEMBA AJIBU HOJA ZA WABUNGE AKIHITIMISHA MJADALA WA BAJETI KUU YA SERIKALI

Written by mzalendo
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), akimpongeza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), baada ya kujibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ambapo jioni, 26/6/2024, wabunge wote watapiga kura, jijini Dodoma. 
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), baada ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kujibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kupigiwa kura na wabunge wote leo jioni, bungeni jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa Serikali itabana matumizi ili fedha zitakazopatikana zielekezwe kwenye miradi muhimu ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akieleza juhudi za Serikali katika kuchochea maendeleo na usimamizi wa fedha wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kupigiwa kura na wabunge wote, bungeni jijini Dodoma leo jioni,
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), akieleza mikakati ya kurahisisha ulipaji wa wakandarasi hususani wazawa wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kupigiwa kura na wabunge wote, bungeni jijini Dodoma, leo jioni. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) akiongoza viongozi wengine wa Wizara ya Fedha kujitambulisha bungeni jijini Dodoma, baada ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kujibu hoja za wabunge akihitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kupigiwa kura na wabunge wote.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)
 

About the author

mzalendo