Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO WIKI YA JUMUIYA YA WAZAZI

Written by mzalendo
MWENYEKITI wa Jumuiya  ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndg.Fadhili Maganya,akizungumza leo Juni 24,2024  Ofisini kwake Jijini Dodoma  na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya Jumuiya ya Wazazi itakayofanyika kuanzia Julai 8 mwaka huu na Kilele chake kitafanyika Julai 13 Mwaka huu katika Wilaya ya Mpanda Mjini Mkoani Katavi.

MWENYEKITI wa Jumuiya  ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndg.Fadhili Maganya,akizungumza leo Juni 24,2024  Ofisini kwake Jijini Dodoma  na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya

wiki ya Jumuiya ya Wazazi itakayofanyika kuanzia Julai 8 mwaka huu na Kilele chake kitafanyika Julai 13 Mwaka huu katika Wilaya ya Mpanda Mjini Mkoani Katavi.
Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya Jumuiya ya Wazazi itakayofanyika kuanzia Julai 8 mwaka huu na Kilele chake kitafanyika Julai 13 Mwaka huu katika Wilaya ya Mpanda Mjini Mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndg.Fadhili Maganya ,ameyasema hayo leo Juni 24,2024  Ofisini kwake Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho  hayo yatakayofanyika katika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele kata ya Inyonga kwenye viwanja vya Shule ya msingi Inyonga.
Bw.Maganya amesema wiki hiyo pamoja na mambo mengine itatumika kupanda miti zaidi ya 100,000 lengo likiwa ni kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kizazi cha sasa na vijavyo.
“Tutakuwa na matukio mengi ikiwemo la Julai  10 ambapo tutakuwa na  Baraza kuu la kawaida la Umoja wa Wazazi Tanzania,Julai  11, Julai Kongamano la maadili na Malezi,na Julai 12  itakuwa maalum kwa ajili ya michezo na kauli mbiu ya Sherehe hizo kwa mwaka 2024 ni Uchaguzi 2024/2025, Jumuiya ya Wazazi iko mstari wa mbele, “amesema Bw.Maganya
Aidha amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi ya CCM, wanaungana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Hassan Bomboko kwa kitendo hicho kwani yeye ndiye msimamizi wa Sheria na Maadili katika wilaya anayoiongoza.
Hatua hii imekuja kufuatia hivi karibuni vyombo vya habari kuripoti kuhusu Sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba ambapo taarifa ilisema limechukua sura mpya, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Hassan Bomboko kupewa notisi ya kuwalipa Sh36 bilioni Mdada poa hao.
Notisi hiyo ya siku 14 inayoanza kuhesabika Alhamisi, Juni 20, 2024, ambayo inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai wamedhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa zaidi ya siku tano kinyume na sheria.
Amesema Jumuiya ya Wazazi ambayo inasimamia maadili kwenye Jamii inamuunga mkoano moja kwa moja Dc wa Ubungo ambaye aliendesha oparesheni ya kuwakamata wanawake hao wanaodhaniwa kuwa madada poa ambao walikutwa katika mazingira ya kuuza miili yao.
“Jumuiya hii tunamuunga mkono DC Hassani kwa Opareshini ile kwani yeye ndiye msimamizi wa sheria katika wilaya yake na alipowakamata hakwenda kama Hassan bali alienda kama kiongozi serikali anapaswa kuhakikisha kunakuwa na maadili katika eneo lake”,amesema

About the author

mzalendo