Featured Kitaifa

DKT. MAHERA ATOA ONYO KWA WASHITIRI WANAOPANDISHA BEI ZA VIFAA TIBA NA KUSAMBAZA VIFAA TIBA FEKI

Written by mzalendo

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Charles Mahera amewakemea washitiri wa vifaa tiba wanaoingiza vifaa visivyokidhi viwango na kuviuza kwa bei ya juu mara tatu zaidi ya bei ya kawaida jambo ambalo linakwamisha juhudi za Mheshimiwa Rais za kutoa huduma bora za Afya kwa watanzania.

Dkt. Mahera ametoa karipio hilo wakati akifungua kikao kazi kati ya TAMISEMI na washitiri wanaosambaza vifaa na vifaa tiba katika maeneo ya kutolea huduma za Afya nchini kilichofanyoka katika ofisi nza TAMISEMI Sokoine House jijini Dodoma.

“Kwa bei za ‘triple’ mara tatu tutawaondoa kwasababu mtakuwa mmeshiriki kuharibu jitihada za mheshimiwa Rais kuhakikisha vifaa na vifaa tiba vinakuwa vingi sasa bei ni milioni tisa nyie mnafanya milioni 18 na suala ubora kuna wengine kama MSD wanasimamia vizuri sana,wengine wanaagizwa kuleta X-Rays wanapewa ‘specification’ wanakwenda kuleta bidhaa feki tunadili na Afya za watanzania hatutaki mzaha katika hili ‘ amesema Dkt. Mahela

Dkt Mahera ameongeza kuwa hivi karibuni Ofisi ya Rais – TAMISEMI itafanya zira ya usimamizi shirikishi katika maeneo mbalimbali nchini na endapo itabaini mapungufu hayo italazimika kuufuta mfumo wa mshitiri.

Hata hivyo,Siku kadhaa zilizopita wataalamu wa Afya kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI walifanya ziara ya usimaizi shirikishi kwenye baadhi ya maeneo nchini na kukuta baadhi ya vifaa tiba visivyokidhi viwango vikiwa kwenye maeneo ya kutolea huduma.

About the author

mzalendo