Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUSHIRIKI SHEREHE ZA UAPISHA WA RAMAPHOSA AFRIKA KUSINI

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kuelekea Jamhuri ya Afrika Kusini leo jioni kwa ziara ya kikazi ya siku moja kushiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo. 

Rais Mteule Matamela Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuapishwa tarehe 19 Juni, 2024. 

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendo