Leo Juni 11, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imefanya mazungumzo na Viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora katika Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi. Ujumbe wa THBUB Mkoani hapo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe.Mohamed Khamis Hamad, ameambatana na Mkurugenzi Msaidizi na Maafisa.
Mhe.Mohamed alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua Maabusu, kusikiliza changamoto za Maabusu, kukagua nyumba za Maaskari, Ofisi na kufanya mazungumzo na Maafisa wa Jeshi hilo.
Kwa upande wa Viongozi hao wameipongeza THBUB kwa kufika Ofisini hapo.
Aidha wameiomba THBUB iendelee kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa askari wa Jeshi la polisi, pia wameiomba THBU kuendelea kufuatilia uboreshaji wa haki na maslahi ya askari hao hususani kupata makazi bora.