Featured Kitaifa

TAMISEMI & UTUMISHI KUSHUGHULIKIa VIBALI VYA AJIRA

Written by mzalendo

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea kushughulikia vibali vya ajira kwa ajili ya kuajiri na kuwapanga wataalam mbalimbali kwenye maeneo yenye upungufu kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshugulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Joseph George Kakunda aliyetaka kujua ni lini Serikali itaipa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Katibu Muhtasi?

Akijibu swali hilo Mhe. Dkt. Dugange amesema “Tayari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kupitia barua ya tarehe 05 Aprili, 2024, imefanya mawasiliano na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ili kujaza nafasi hiyo na tayari Mwandishi Mwendesha Ofisi amesharipoti na kuanza kazi tarehe 08/04/2024”. Amesema

Dkt. Dugange ameongeza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha ofisi za wakuu wa wilaya kote nchini na ofisi zingine zote zinakuwa na wataalamu wanaohitajika ili kukidhi huduma zote zinazohitajika kutolewa.

About the author

mzalendo