Featured Michezo

KIGOMA YAILIZA PWANI MPIRA WA GOLI

Written by mzalendo

TIMU ya Mkoa wa Kigoma
imeibuka na ushindi dhidi ya mkoa wa Pwani, baada ya kuifunga jumla ya magoli 10-0 katika mchezo ya mpira wa Goli wasichana, kwenye mashijdano ya UMITASHUMTA yanayofanyika kitaifa mkoani Tabora.

Katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye ukumbi wa Chuo cha Uhazili Tabora, timu ya Mkoa wa Njombe wasichana iliifunga Mwanza kwa magoli 10-0, na Dodoma ikaibuka kidedea kwa kuifunga Rukwa magoli 8-3

Kwa upande wa wavulana Kigoma imeifunga Pwani kwa magoli 10-0 huku Mwanza ikiifunga Shinyanga magoli 10-0

Mpira wa goli ni mchezo unaohusisha wachezaji wenye uono hafifu huku jumla ya Mikoa 23 kutoka Tanzania Bara na Visiwani ikishiriki mashindano hayo mwaka huu.

Lengo kuu la michezo hii maalum, ni kuhakikisha kuwa mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA yanakuwa jumuishi kwa kuweka fursa ya kushiriki kwa wanafunzi wote.

About the author

mzalendo