Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Soko la Samaki la Kisasa la Chato Beach katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita, Juni 3, 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Nicholas Kasandamila, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, wa pili kulia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Cyprian Manonga. (Piicha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………….
Waziri Mkuu Kassim Majakiwa amesema Serikali inaendelea kujikita katika kuhakikisha inaimarisha na kuwashirikisha wavuvi na wafugaji katika mipango ya maendeleo.
Amesema hayo leo Juni 03, 2024 alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la samaki la kisasa la Chato Beach, Chato mkoani Geita.
Amesema kuwa Mradi huo unaotoa fursa kwa yeyote aliyeanza na anayetaka kujikita kwenye sekta ya uvuvi kunufaika na kujiingizia kipato. “Kitendo cha Serikali kuleta soko hili hapa ni kuhakikisha wanasogeza fursa kwa wavuvi wa eneo hili, soko hilo ni lenu, imarisheni uchumi wenu kupitia soko hili”.
Ameongeza soko hilo litakuwa na uwezo wa kukausha hadi tani 10 za dagaa kwa siku kwa kuwa kutawekwa mtambo wa kukausha samaki. “Tutaweka mafriji makubwa mawili ya kutunzia samaki, pamoja na chumba maalum cha kuzalisha barafu”
Ujenzi wa soko hilo ambalo umefikia asilimia 90 utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.75 na utasaidia kupunguza upotevu wa samaki hasa dagaa baada ya kuvunwa, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kutoa ajira zipatazo 1473 kwa wavuvi, wafanyabiashara na wachuuzi na kuimarisha ukusanyaji wa takwimu za uvuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Samaki la Chato Beach kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo katika mji mdogo wa Chato Mkoani Geita Juni 3, 2024. Kulia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani na wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Paskazia Gervas (kushoto) ambaye ni mmoja wa wachuuzi wa samaki kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Soko la Kisasa la Samaki la Chato Beach katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita, Juni 3, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Soko la Kisasa la Samaki la Chato Beach lililopo kwenye mji mdogo wa Chato mkoani Geita, Juni 3, 2024. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Agness Simon (kushoto) na Sabina Alfred ambao ni wachuuza samaki kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Soko la Kisasa la Samaki la Chato la Beach katika mji modogo wa Chato mkoani Geita, Juni 3, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)