Featured Kitaifa

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MAJENGO YA UTAWALA-MAJALIWA

Written by mzalendo

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Geita, Juni 2, 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka  jiwe la msingi la jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Geita, Juni 2, 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Muonekano wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita ambalo Waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake, Juni 2, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa Sabasaba uliopo Karumwa wilayani Nyang’hwale, mkoa wa Geita,  kuhutubia mkutano wa hadhara, Juni 2, 2024.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

Waziri kuu, Kassim Majaliwa akizindua jengo la Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita, Juni 2, 2024. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajasiliamali waliowezeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzindua Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililopo Karumwa wilayani Nyang’wale mkoani Geita, Juni 2, 2024. Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingarame. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo za batiki alipotembelea banda la maonesho la wanawake wajasiriamali waliowezeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzindua kituo cha baraza hilo kilichopo Karumwa wilayani Nyang’wale mkoa wa Geita, Juni 2, 2024.   Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng’i Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Rehema Mwakalanga alipotembelea banda la maonesho la wanawake wajasiriamali waliowezeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzindua kituo cha Baraza hilo kilichopo Karumwa wilayani Nyang’hwale mkoa wa Geita, Juni 2, 2024.   Wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng,i Issa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

default

default

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi kwenye uwanja wa Sabasaba uliopo Karumwa wilayani Nyang’hwale mkoani Geita, Juni 2, 2024. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

…..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ataendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha majengo ya utawala kwenye halmashauri zote nchini ikiwemo na ya wilaya ya Nyang’hwale.

Amesema ujenzi wa majengo hayo ya kutolea huduma kwa wananchi ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ambayo imeielekeza Serikali kujenga miundombinu hiyo muhimu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Juni 02, 2024) baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyangh’hwale ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85 na umegharimu sh bilioni 3.7.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ataendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha majengo ya utawala kwenye halmashauri zetu lengo likiwa ni kuona wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao”

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Idara na watumishi wote waendelee kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa katika kuwahudumia wananchi “Wananchi wana matumaini makubwa na Serikali yao, wahudumieni na mtatue kero zao.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale, Husna Toni amesema mradi huo utakapokamilika utaboresha mazingira ya kufanya kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi kwenda katika halmashauri yao kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali zikiwemo na za kumalizia ujenzi wa jengo hilo ulioanza 2017/2018.

Baada ya kuweka jiwe na msingi la jengo la halmashauri, pia Waziri Mkuu amezindua jengo la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo litawawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kupata huduma mbalimbali ikiwemo elimu ya biashara na ujasiriamali.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo ambalo limejengwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakazi wa eneo hilo kutumia fursa kituo hicho kwa ajili ya kupata elimu ya biashara na ujasiriamali pamoja na mikopo ili wajiendeleze kiuchumi.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi hao kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali. “Vikundi vinakopesheka kwa urahisi hata anuani yake ni rahisi”.

Naye, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa kituo hicho kwani kitatoa fursa ya wafanyabiashara na wajasiriamali kupata elimu sahihi ya mikopo na kujiepusha na mikopo umiza.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga ameahidi kuendelea kusimamia ujenzi na uendelezaji wa vituo hivyo katika maeneo mengine nchini ili viweze kuleta tija kwa wananchi.

Awali, Mkuu wa wilaya hiyo, Grace Kingalame alimshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuidhinisha utoaji wa fedha ambapo katika wilaya yao wamepokea zaidi ya sh bilioni 25 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema kati ya fedha hizo shilingi tisa zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini na tayari vijiji vyote vya wilaya hiyo vimepata umeme, pia zaidi ya shilingi bilioni 6.8 zimepelekwa katika utekelezaji wa miradi ya maji.

About the author

mzalendo