Featured Kitaifa

WHI YANG’ARA TUZO ZA ACOYA 2024

Written by mzalendoeditor

 

Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) imeshinda tuzo ya Fund Manager of the Year 2024 katika tuzo za Africa Company of the Year Award (ACOYA) zilizoandaliwa na The Global CEO Institute usiku wa leo tarehe 31/05/2024 katika ukumbi wa Super Dome Tz (Masaki). WHI ni taasisi inayosimamia mifuko miliwi ya uwekezaje Mfuko wa Nyumba na Mfuko wa uwekezaji wa pamoja kwenye masoko ya fedha na mitaji unaitwa Faida Fund. Huu ni mfuko unaoruhusu watanzania wote wenye kipato cha chini,kati na juu kuwekeza kwa lengo kubwa la kuuza mitaji au kujiongezea kipato kupitia uwekezaji wa pamoja.
Katika tuzo hizi nchi nane (8) kutoka barani Afrika zimeshiriki.

Hongereni sana Watumishi Housing Investments.

#AfricaCompanyoftheyear
#Award2024

About the author

mzalendoeditor