Featured Kitaifa

MAKUMBUSHO INAYOTEMBEA YATINGA BUNGENI – DODOMA

Written by mzalendo

Na Sixmund Begashe, Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa, imeweka onesho adimu la vioneshwa vya urithi wa asili na utamaduni ndani ya viwanja vya Bunge, kupitia gari Maalum, kwa lengo la kuelezea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo kupitia Taasisi ya Makumbusho.

Akikagua maonesho hayo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ameipongeza Idara ya Malikale kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa ubunifu makubwa wa Makumbusho hiyo inayotembea

Mhe. Kairuki ameagiza
hamasa ifanyike zaidi hasa kwenye maonesho hayo ili Waheshimiwa Wabunge waweze kushirikiana na Makumbusho, kuwafikishia maonesho hayo ya Kimakumbusho wananchi kwenye maeneo yao.

Aidha, katika kuelekea uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya Mwaka 2023/2025, Wizara hiyo imeweka maonesho mbalimbali hususan ya Wanyama hai, Makumbusho inayotembea, nyama choma za Wanyamapori , kwenye viwanja vya Bunge ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa Waheshimiwa Wabunge na wagani mbalimbali wanaofika Bungeni.

About the author

mzalendo