Featured Kitaifa

TUWAKEMEE WENYE KUTAKA KULIGAWA TAIFA – DK NCHIMBI

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amekemea kundi la watu lenye nia ya kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ukabila na maeneo ambapo amesisitiza watu hao wanapaswa kukemewa.

Amesema Watanzania hawafurahishwi na kauli hizo zenye lengo la kuleta magawanyiko kwani Tanzania imejengwa kwa umoja na mshikamano bila ubaguzi.

Dk. Nchimbi alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mji wa Manyoni mkoani Singida ikiwa ni siku ya kwanza katika mikoa mitano iliyoanzia mkoani hapa.

“Kuna watu wameanza kuongelea ukabila, baadhi ya watu wameanza kuongelea Tanzania Bara na Zanzibar. Wapo wanaozungumza kwamba Watanganyika hatunufaiki na muungano.

“Wapo wanaosema Wazanzibar hatunufaiki na muungano. Watu wanashabikia mgawanyo wa watu kwa misingi ya ukabila au maeneo kwa kujua au kutojua. Tunakwenda kuligawa taifa letu,” alieleza.

About the author

mzalendoeditor