Featured Kitaifa

MRADI WA DMDP II KUJENGA BARABARA KM 42 BARABARA ZA LAMI, KIGAMBONI

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amesema Serikali inatekeleza mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP II) na unahusisha ujenzi wa kilomita 42.1 za barabara za lami kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, mifereji ya maji ya mvua pamoja na madaraja.

Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni aliyeuliza Je, kuna mkakati gani wa Serikali kuongeza wigo wa barabara za lami katika Wilaya ya Kigamboni?

“kwa mwaka 2023/24, Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ilitenga shilingi bilioni 2.88 ambazo zilitumika kujenga barabara ya Tungi – Mjimwema na Chagani Polisi (kilomita 2.3) na mifereji yenye urefu wa mita 3,800. Mwaka 2024/25 zimetengwa shilingi bilioni 2.215 ambazo zitatumika kujenga barabara ya Rombo Bar – RC Church Kivukoni, Kivukoni P/S na umaliziaji wa Barabara ya Chagani – Polisi kwa kiwango cha lami kilomita 1.52 na mifereji yenye urefu wa mita 3,040” Mhe. Katimba.

Amesema pia Serikali inatambua umhimu wa Barabara za lami katika Miji na itaendelea kujenga Barabara hizo pia kuziboresha kwa kuziwekea wigo Barabara hizo zikiwemo za Manspaa, na Majijii li ziendelee kuwasaidia wanachi.

Mradi huu wa DMDP II kwa Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam utajenga barabara za Lami zenye urefu wa KM 253.

About the author

mzalendo