Kimataifa

HELIKOPTA YA RAIS WA IRAN IMEPATIKANA

Written by mzalendo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya “Red Crescent” Iran, Kolivand, ametangaza kuwa mabaki ya helikopta iliyokuwa imembemba Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian, na maafisa wengine kadhaa yamepatikana.

Helikopta hiyo ilipatikana kaskazini magharibi kwenye mteremko wa kilima katika eneo la Varzaghan, karibu na mpaka wa Azerbaijan Mashariki.

Mapema saa saba hadi nane zilizopita iliripotiwa kuwa ndege hiyo imepata ajali na wataalamu walianza kuisaka mara moja huku hali mbaya ya hewa ikitajwa kama chanzo cha ajali hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti ya awali ya mwenyekiti wa Red Crescent, hakuna dalili za uhai wa watu kwenye ajali hiyo.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri taarifa zinavyothibitishwa.

Chanzo: Azam tv

About the author

mzalendo