Featured Kitaifa

SERIKALI KUONGEZA SHULE ZA SEKONDARI KIDATO CHA TANO NA SITA

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) Serikali imefanya jitihada za kujenga na kupanua shule za Sekondari za kidato cha Tano na Sita za kitaifa ili kukidhi uwepo wa idadi kubwa ya Wanafunzi wanaotokano na utekelezaji wa Sera ya Elimu bila Malipo.

Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Hanang` Mhe. Samwel Xaday Hhayuma alieuliza Je lini serikali itapandisha hadhi Shule za Sekondari Simbay, Sumbaye na Mary Nagu zilizopo Hanang kuwa kidato cha Tano na Sita?

“Idadi ya shule za kidato cha Tano na Sita imeongezeka kutoka 318 mwaka 2016 hadi shule 613 kwa mwaka 2024 ambao ni sawa na ongezeko la 48.2%, Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kujenga na kupanua shule za Sekondari za kidato cha Tano na Sita za kukidhi uwepo wa idadi kubwa ya Wanafunzi wanaotokano na utekelezaji wa Sera ya Elimu bila Malipo.” Mhe Katimba.

Amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali kupitia Mradi wa SEQUIP imepanga kujenga Shule za Bweni za Wavulana za kitaifa 7 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi, pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Shule za Sayansi za Wasichana za Bweni 26.

Aidha Mhe. Katimba amesema Serikali inatambua umhimu wa Utaifa kuanzia katika utoaji wa Elimu hasa katika kidato cha Tano na Sita kuwa za Kitaifa na kuboresha Miundombinu bora kwani shule hizi hupokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali Nchini hii inasababisha kudumisha Umoja na Mshikamano miongoni mwa wanafunzi.

About the author

mzalendo