Featured Kitaifa

BIL. 322.3 ZATENGWA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA NGAZI YA AFYA MSINGI

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange (Mb) amesema Serikali imetenga jumla ya shilingi Bil. 322.3 kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya huduma za Afya katika ngazi ya Afya Msingi.

Kati ya fedha hizo shilingi Bil. 205 ni kwaajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi na shilingi Bil. 117.3 kwaajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa Tiba ngazi ya msingi ili kuboresha huduma za Afya.” Dkt. Dugange

Dkt.Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ghati Zephania Chomete (Mb) aliyeuliza Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha dawa zinapatikana na kukidhi mahitaji katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Mkoa wa Mara.

Aidha Dkt Dugange amesema Wastaafu wanahaki ya kupata Matibabu kupitia Bima, amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar, Mhe, Asha Abdallah Juma aliyetaka kujua Je ni lini Serikali itawasaidia Wastaafu ambao wameambiwa Bima zao zimeshitishwa?

“Ni haki ya Wastaafu kuendelea kupata huduma za Afya kupitia Bima, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara Afya imelichukua swala hili na kufuatilia na kulifanyia kazi ili wastaafu wote wapate haki yao ya Matibabu” Dkt. Dugange.

About the author

mzalendo