Featured Kitaifa

KATAMBI ATETA NA MENEJIMEMNTI PAMOJA NA WAKUU WA TAASISI

Written by mzalendoeditor

Na; Mwandishi Wetu – Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekutana na Menejimenti ya Ofisi hiyo pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika Mwenendo wa ulipaji Mafao, Uwekezaji wa mifuko na tathmini ya uhai wa mifuko.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 4, 2024 kwenye ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma.

Aidha, Mheshimiwa Katambi ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuendelea kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama sambamba na kuendelea kulipa mafao kwa wakati.

About the author

mzalendoeditor