Featured Kitaifa

BILA MPANGO MZURI WA KUONGEZA THAMANI MADINI HUPATI LESENI

Written by mzalendo

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kwasasa hawatatoa Leseni ya Kati (ML) na Kubwa (SML) ya Uchimbaji wa madini yote yakiwemo madini mkakati na madini muhimu kwa Mwekezaji yoyote kama hatokuwa na mpango mzuri wa kuongeza thamani madini hapa nchini, lengo likiwa ni kuifanya Tanzania kunufaika na rasilimali madini iliyonayo.

Mavunde ameyamesema hayo leo Aprili 30,2024 Bungeni Jijini wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha amesema ili kuimarisha Ukusanyaji wa Maduhuli na kuongeza Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la taifa Wizara imepanga kuhamasisha kuanza kwa uzalishaji kwa kampuni zilizopewa leseni za uchimbaji, usafishaji na biashara ya madini na kuimarisha usimamizi wa migodi ya uchimbaji madini.

Sambamba na hayo, ameongeza kuwa Wizara
itaendelea kuimarisha udhibiti wa vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na biashara haramu ya madini nchini kwa kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa shughuli za uchimbaji wa madini kwa kununua wa vitendea kazi kama magari na pikipiki kwa ajili ya mikoa yote ili kuongeza ufanisi wa kazi

About the author

mzalendo