Featured Kitaifa

DCEA KANDA YA KASKAZINI:UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE MOSHI KILIMANJARO

Written by mzalendo
Na Prisca Libaga Kilimanjaro
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini leo tarehe 23 Aprili 2024 imefanya ziara Mkoani Kilimanjaro.
Lengo la ziara hii ni kujitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kumuelezea uwepo wa Ofisi za  Mamlaka Kanda ya Kaskazini na Kazi zake, pamoja na kuomba ushirikiano wa karibu na Ofisi yake ili kuweza Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Pamoja na hilo Maafisa kutoka Mamlaka Kanda ya Kaskazini imetembelea na kuzihakiki Asasi zinazofanya kazi ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya sambamba na Kuibua Asasi nyingine zinazotoa huduma kwa makundi ambayo yapo kwenye hatari ya kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha katika kutekeleza Makubaliano kati ya PCCB na DCEA, Maafisa kutoka Mamlaka wameungana na Afisa kutoka TAKUKURU Kilimanjaro kutoa Elimu kwenye shule ya MJI MPYA iliyoko Kata ya Majengo sambamba na kuhamasisha Klabu ya shule hiyo ili iweze kutoa Elimu juu ya Madhara ya Matumizi ya Dawa za Kulevya na Kupiga vita Rushwa.
Elimu kwa UMMA ilitolewa na Maafisa wa Mamlaka Kanda ya Kaskazini, Afisa wa TAKUKURU na Mwanasaikolojia kutoka Asasi ya Kiraia kwenye kituo cha Redio cha BANANA FM sambamba na kuhamasisha Jamii kutoa Taarifa kwenye namba za 119 na 113 ili kupata Uelewa sahihi juu ya Kupinga Rushwa na Dawa za Kulevya.
“PIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KWA USTAWI WA JAMII”

About the author

mzalendo