Featured Kitaifa

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA ELIMU DHIDI YA  RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA

Written by mzalendo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati akizidua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora,hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora.

MKUU  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma John Joseph ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora.

MKUU Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora.

BAADHI ya washiriki katika  mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora,hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI  imesema  itaendelea kushirikiana na  ngazi zote za elimu katika kupambana na Rushwa na Dawa za kulevya.

Hayo yalibanishwa jijini Dodoma na Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene ,wakati akizidua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi Sekondari,Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kuhusu Madhara ya Rushwa,Matumizi ya Dawa za Kulevya,Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Alisema serikali za awamu zote zimefaikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, umaskini maradhi kwa Watanzania.

“Sasa wameibuka maadui wengine watatu ambao ni rushwa, dawa za kulevya na maadili ambao kuna kazi kubwa ya kufaya kuhakikisha tunatokomeza, hili sio suala la kuachia serikali pekee ni vyema kila mwananchi akashiriki kikamilifu,”alisema

Aliogeza kuwa:”Leo ninafurahi kuzindua mdahalo huu kwa shule na vyuo vya Dodoma kuhusu masuala ya rushwa ni jambo jema kwasababu ndio msingi imara wa kuandaa viongozi wazalendo na ningetamani kuona kitu kama hiki kiafanyika nchi nzima,”.

Simbachawene alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweli kwa kuandaa midahalo hiyo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi wa ngazi zote za elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.John Joseph alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athali za rushwa hasa katika miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao.

Alisema pia wameedelea kuanzisha klabu za wapinga rushwa kuanzia shule za msingi hadi vyuo lengo ni kuongeza mtandao wa kupokea taarifa za rushwa na kutoa elimu kwa kudi hilo la vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

“Tunaendelea kufungua klabu za wapinga rushwa lengo ni kuhakikisha tunalifikia kundi kubwa la vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa ambapo tunaamini tukiwaelimisha wao tutakuwa tumeelimisha Taifa,”alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri alisema lengo la kuanzisha midahalo hiyo ni kuhakikisha watu wanapata uelewa wa kutosha kuhusu athali za rushwa.

“Watu wengi wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kwasababu ya vitendo vya rushwa na ndio kitu kikubwa kilichonisukuma kuanzisha jambo hili ambalo hadi sasa limeonyesha matunda makubwa,”alisema

Awali Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Bunge Mariamu Minja alisema midahalo hiyo imekuwa na manufaa kwao kwasababu inawafundisha ni kwa namna gani wanatakiwa kuwa wazalendo.

“Tunamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kwa kuja na wazo hilo kiukweli limekuwa na manufaa kwetu tunaomba isiishie mjini hata wanafunzi walioko vijijini nao wapate fursa ili wapate elimu na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya rushwa,”alisema

About the author

mzalendo