Mkurugenzi wa Huduma za Afya,Ustawi wa jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ametoa muda wa wiki mbili kwa timu ya usimamizi wa huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) ya Misenyi kujitafakari kiutendaji kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ikiwemo kushindwa kusimamia makusanyo ya mapato katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo wakati wa kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Misenyi mkoa wa Kagera akiwa ameambatana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambapo amebaini Hospitali hiyo iliyoanza kufanyakazi tangu mwakwa 2022 kutokuwa na taarifa ya makusanyo ya fedha kwa miezi sita tangu mwezi Novemba 2023.
“kwingine tulikopita tumeambiwa wanatibiwa wamama wajawazito na Watoto wachanga tu tukawaambia waache upuuzi tumekuja hapa tunaambiwa tunaambiwa wanaotibiwa ni miradi misonge (maralia,HIV na mengine) kitu ambacho hatuwezi kudanganywa kwa namna hiyo” Amesema Dkt. Rashid mfaume
Aidha,Dkt. Mfaume ametoa maelekezo kwa waganga wakuu wa mikoa na Halmashauri zote nchini kufuatilia nakusanyo kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ya Msingi ili yaliyojitokeza katika Hospitali mpya ya Misungwe na Misenyi yasijitokeze.