Featured Kitaifa

MCHIMBA MADINI AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUMFUNGIA KINYUMBA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

Written by mzalendo

Mahakama ya Wilaya ya Songwe mkoani Songwe tarehe 08 April 2024 imemhukumu mshtakiwa Shomari Hamis kwajina maarufu Kijasho Ras (28) Mchimbaji wa Madini, mkazi wa Patamela kata ya Saza, kutumikia adhabu ya Kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa April 01, 2024 maeneo ya Kata ya Saza wilayani Songwe ambapo alituhumiwa kumfungia mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 nyumbani kwake na kumbaka mpaka majirani walipomfunguliwa mwanafunzi huyo baada ya kusikia kelele kutoka kwenye nyumba hiyo, kitendo hicho ni kosa la jinai ambalo ni kinyume na kifungu cha 130 (2) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 ya mwaka 2022.

Akisoma maelezo ya hukumu ya kesi hiyo yenye kesi namba 23/2023 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Songwe Mheshimiwa Lefi Sizya alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa la kubaka na kumhukumu adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

About the author

mzalendo