Na. Asila Twaha, OR-TAMISEMI
Mkurugenzi Msaidizi huduma za Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje ameishauri jamii kushiriki katika suala la malezi na makuzi ya watoto kupitia vituo vya kulelea watoto.
Amesema hayo Aprili 8, 2024 wakati alipotembelea Vituo vya kulelea watoto wadogo vilivyopo Bahi Sokoni na Mundemu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Amesema lengo la Serikali kujenga vituo vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto chini umri wa miaka mitano ni kwa ajli ya kuwapatia watoto huduma za melezi, makuzi ya awali uchangamshi kwa katika maeneo ya Afya, lishe, ujifunzaji wa awali, malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.
Bi.Kabuje amesema ni vizuri jamii kuwa na ushirikiano na Serikali kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa endelelevu kwa jamii, wazazi na walezi kusaidia watoto hasa katika mahitaji muhimu ikiwemo kuchangia suala la upatikani wa chakula katika vituo hivyo kwani husaidia sana katika malezi na makuzi ya watoto.
Naye Mlezi wa kituo cha Bahi Sokoni Witness Omary amesema Serikali iendelee kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa malezi ya mtoto na jukumu la kulea watoto ni jukumu la jamii hivyo ni vizuri kushirikiana kwa pamoja ili kuwawezesha watoto kufikia malengo yao.