Featured Kitaifa

WAZIRI NDEJEMBI ATAKA MATOKEO CHANYA KATIKA UTENDAJI KAZI

Written by mzalendo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masula ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa serikali Mtumba leo Aprili 5, 2024 kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 4 Aprili, 2024. 

  

Sehemu ya menejimenti na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa serikali Mtumba leo Aprili 5, 2024 kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 4 Aprili, 2024.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo mara baada ya kumpokea rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Deogratius Ndejembi na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Mhe. Mary Ngelela Maganga. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Deogratius Ndejembi. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Mary Ngelela Maganga.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Mary Ngelela Maganga akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa ofisi hilo alipowasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa serikali Mtumba leo Aprili 5, 2024, jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masula ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Mhe. Mary Ngelela Maganga mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa serikali Mtumba leo Aprili 5, 2024 kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 4 Aprili,

Na; Mwandishi Wetu – DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masula ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa Ofisi yake kuimarisha utendaji kazi ili kuleta matokeo chanya na yenye tija katika kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema, Wizara hiyo ni kubwa na wananchi wanatarajia makubwa kupitia sekta inazozisimamia ikiwemo masuala ya maendeleo ya Vijana, Ajira, ustawi wa Watu wenye Ulemavu, Wafanyakazi, Waajiri na Wastaafu.

Amesema hayo leo Aprili 5, 2024 wakati alipowasili kwenye hiyo Ofisi  iliyopo Mji wa serikali Mtumba kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 4 Aprili, 2024.

Vile vile, Mhe. Ndejembi amehamasisha menejimenti na watumishi wa Ofisi yake kuhakikisha wanasimamia maelekezo na miongozo yanayotolewa na viongozi wakuu wa serikali kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika utendaji kazi.

Kwa upande mwengine, Waziri Ndejembi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Waziri katika Ofisi hiyo na kuahidi kushirikiana na watumishi wa Ofisi yake ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Akizungumza awali, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mhe. Waziri na Katibu Mkuu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri Ndejembi amewasili katika ofisi yake ambapo alipokelewa na Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu, Mhe. Mary Ngelela Maganga.

About the author

mzalendo