Featured Kitaifa

SILAA,MCHENGERWA BEGA KWA BEGA KUTATUA KERO ZA ARDHI

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka watumishi wa Sekta ya Ardhi kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa uadilifu na upendo kwani hayo ndio maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kumaliza shida za watanzania katika ardhi zinaisha.
 
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Iftar iliyoandaliwa na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Dar es salaam amesema kupitia wizara yake atahakikisha anashirikiana na Wizara ya ardhi ili kumaliza kero za ardhi.
Iftar hiyo imeandaliwa kwa lengo lengo la kuwakutanisha pamoja watumishi wa Sekta ya Ardhi, Wananchi wa Jijini Dar es salaam pamoja viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali katika viwanja vya ofisi ya Kamishna wa Ardhi mkoa wa Da es salaam Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor