Featured Kitaifa

TACAIDS YALIOMBA BUNGE KUHIDHINISHIWA BILIONI 17.8

Written by mzalendo

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya Mhe. Stanslaus Nyongo ameliomba Bunge kuhidhinisha kiasi cha Bilioni 17.8 kwaajili ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ambapo 4.5 ni kwaajili ya matumizi ya kawaida na Bilioni 13.2 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2024/2025.

Mhe. Nyongo ametoa ombi hilo leo Aprili 3,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati wakati akiwasilisha maoni ya kamati kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TACAIDS) kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Aidha amesema baada ya uchambuzi wa Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na makadirio ya Matumizi kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania ameshauri upatikanaji wa Fedha za Ndani kwa ajili ya afua za UKIMWI.

“Serikali itoe fedha zote za Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kama zilivyoidhinishwa na Bunge ili kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa,”amesema.

Aidha ameiomba Serikali kuimarisha Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI na kuweka mipango madhubuti ya kupata vyanzo mahsusi vya mapato ya ndani

vitakavyosaidia kupata fedha zaidi kwa ajili ya miradi inayolenga kudhibiti VVU na UKIMWI.

About the author

mzalendo