Featured Kitaifa

SERIKALI YAAHIDI KUONGEZA KASI YA UTATUZI WA MIGOGORO KUPITIA TUME INAYOTEMBEA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kuongeza kasi ya kutatua migogoro ya kikazi, kwa kusogeza huduma karibu na wafanyakazi na waajiri kupitia tume inayotembea yaani “Mobile Labour DisputesSettlement Services”.

Ameyasema hayo leo Aprili 03, 2024, Bungeni wakati akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na Ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Vilevile, amesema Serikali imeendelea kutatua migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi ambapo mpaka kufikia Februali, 2024 jumla ya migogoro 2,712 imetatuliwa ambapo Migogoro 4,579 ilipokelewa.

About the author

mzalendo