Kimataifa

15 WAUWAWA SUDAN KUSINI NA VIJANA WALIOKUWA WAMEJIHAMI NA SILAHA

Written by mzalendo

Afisa wa ngazi ya juu wa Sudan Kusini amesema Jumatano  kwamba vijana waliokuwa wamejihami wameua watu 15 kwenye jimbo la Pibor, akiwemo mkuu wa Kaunti, wakati hali ya taharuki ikiendelea kuongezeka nchini humo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.

Mauaji hayo ya bunduki yameripotiwa kutokea Jumanne, pale kamishna wa kaunti ya Boma, iliyopo jimbo la Pibor, alipokuwa akirejea mjini, baada ya kutembelea kijiji chake. Ghasia zilizozuka miaka miwili baada ya kujipatia uhuru kutoka kwa Sudan zilisababisha vifo vya maelfu ya watu kati ya 2013 na 2018.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hali ya utulivu imeshuhudiwa tangu wakati huo, ingawa kumekuwa na ghasia miongoni mwa makundi yenye silaha kwenye sehemu tofauti za nchi. Wanaharakati wanasema kwamba ongezeko la ghasia la hivi karibuni huenda ni kutokana na uchaguzi ujao ambapo wapiga kura watachagua viongozi watakaorithi utawala wa sasa wa mpito.

About the author

mzalendo