Featured Kimataifa

KIM AVITAKA VIKOSI VYA ULINZI KUJIWEKA TAYARI KWA VITA

Written by mzalendo

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, ametoa wito kwa vikosi vya jeshi la nchi hiyo kujiweka tayari kikamilifu kukabiliana na mzozo wowote unaoweza kutokea.

Kim ametoa wito huo wakati alipohudhuria mazoezi ya vikosi vya Jeshi la Anga la nchi hiyo, ambapo ametilia mkazo kuwa jukumu la msingi la jeshi ni kujiandaa kwa ajili ya vita na ameviagiza vikosi vya Jeshi la Anga vya nchi hiyo kujiweka tayari kutekeleza mbinu mbalimbali za vita za kushangaza.

“Vikosi vyetu vipasa kuwa tayari kukabiliana na adui kwa ari na nguvu zote na kubadilisha historia katika tukio la vita”, amesema Kiongozi wa Korea Kaskazini bila kutaja nchi yoyote kuwa tishio tarajiwa kwa nchi hiyo. Huku nyuma, Kim Jong-un aliwahi kutoa miito sawa na huu na kuituhumu Marekani kuwa inaisukuma Peninsula ya Korea katika vita. 

Korea ya Kaskazini tangu mwaka jana imefanyia majaribio makombora yake kadhaa ya cruise na ya balistiki ikidhihirisha uwezo wake mkabala wa sera za Marekani katika Peninsula ya Korea. Pyongyang inasema sera hizo za Washington zinafanya suala la vita kutoepukika.”

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini aidha ametaja mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka kati ya  Seoul na Washington kuwa yanafanyika kwa ajili ya kukivamia nchi yake.

About the author

mzalendo