Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAUPONGEZA MKOA WA MANYARA UNAVYOSIMAMIA UJENZI WA SHULE YA WASICHANA

Written by mzalendo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeupongeza Uongozi wa Mkoa wa Manyara kwa namna inavyosimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Mkoa inayojengwa katika Kijiji cha Kiongozi, Halmashauri ya Mji wa Babati huku ikitoa rai ya kusimamia utunzwaji wa miundombinu ya shule hiyo pindi itakapokamilika.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dennis Londo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye halmashauri hiyo iliyoanza tarehe 12.03.2024.

“ Kipekee kabisa niupongeze Mkoa wa Manyara kwa kazi kubwa mliyofanya ya kusimamia kwa weledi ujenzi wa shule hii ya wasichana ya mkoa huu. Hapa thamani ya fedha inaendana na ujenzi wenyewe.

Shule hii ni rejea ya shule zingine ambazo zinajengwa nchini, tumepita maeneo mengi na kwa hakika tumeridhishwa na ujenzi wa shule hii, niwatake viongozi wa mkoa na wananchi kwa ujumla mnalinda miundombinu ya ujenzi huu ili iweze kudumu na kutumika na vizazi vingi zaidi,” Amesema Mhe Londo.

About the author

mzalendo