Featured Kitaifa

EWURA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WILAYANI CHAMWINO

Written by mzalendo
MWEYEKITI  wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima  akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA waliojitokeza katika maandamano kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika   Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma leo Machi 8,2024.
Baadhi ya Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakishangilia katikati ya viwanja vya Chinangali II jijini Dodoma eneo ambalo maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanafanyika Kitaifa.
Baadhi ya Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani)  katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Chinangali II wilayani Chamwino mkoani Dodoma
MWEYEKITI  wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima,akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kushiriki  Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
MWEYEKITI  wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima (kushoto),akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA wakikabidhi hundi ya sh.Milioni tano katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino wakati wa Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
MWEYEKITI  wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima pamoja na Wafanyakazi Wanawake wa EWURA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi   hundi ya sh.Milioni tano katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino wakati wa Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Na Alex Sonna-CHAMWINO
WAFANYAKAZI Wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wametembelea Shule ya Msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri wilayani Chamwino na kutoa hundi ya Sh.Milioni tano ili kusaidia kununua vitu mbalimbali ikiwamo karatasi za nukta nundu.
Akizungumza leo baada ya kutembelea shule hiyo, Mwenyekiti wa wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA, Herieth Kasilima, amesema fedha hiyo pia itanunua chakula.
Herieth amehimiza taasisi zingine kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kutokana na kuwa na mahitaji mengi ili watoto hao wafikie ndoto zao kielimu.
Pamoja na kutoa msaada huo, wanawake hao wameungana na wengine katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa mkoani Dodoma katika Wilaya ya Chamwino.
Katika hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima, amesisita matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia ambapo EWURA wanajukumu la kudhibiti huduma ya nishati ya gesi.

About the author

mzalendo